Wanamuziki kutoka Nigeria kwa mara nyengine tena wamewika katika sherehe za tuzo za MTV Awards mwaka 2015 zilizoandaliwa katika eneo la KwaZulu-Natal ikinchini Afrika kusini. Tuzo hizo ziliwaleta pamoja wasanii wa ubunifu na muziki kutoka barani Afrika huku wengine wakifanya maonyesho ya muziki uliowavutia wengi. Wale walioshinda usiku huo ni wasanii wa Nigeria akiwemo Yemi Alade na Davido ambao walijishindia tuzo za mwanamuziki bora wa kike na wakiume mtawalia huku nyota wa hip hop Cassper Nyovest akijishindia taji la mwanamuziki bora wa mtindo wa hip hop. D'Banj naye alishinda tuzo la mageuzi,likiwa ni tuzo jipya ambalo hupewa wanamuziki wa siku nyingi ambao wamewika katika utamaduni wa muziki wa Afrika. Wawakilishi wa eneo la Afrika mashariki akiwemo msanii Diamond kutoka nchini Tanzania alishinda tuzo la Best Live music huku Sauti Sol Wakenya wakishindwa kupata tuzo lolote. Nicki Minaj alishinda tuzo la mwanamuziki bora wa kimataifa huku kundi la P sq...